

Lugha Nyingine
Wanajeshi wawasili Los Angeles licha ya upingaji kutoka kwa viongozi wa eneo hilo
Shirika la Habari la ABC la Marekani limeonesha video za wanajeshi wa Marekani waliotumwa na serikali ya Rais Trump wakiwasili mjini Los Angeles katika Jimbo la California.
Hii ni mara ya kwanza tangu mwaka 1965 kwa rais kuamrisha kikosi cha walinzi wa taifa bila ombi kutoka kwa gavana wa jimbo husika.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mivutano kati ya waandamanaji wanaopinga vitendo vya maofisa kutoka Idara ya Uhamiaji ya Marekani (ICE) na mashirika mengine kusimamia utekelezaji sheria ya Marekani kuvamia maeneo kadhaa kusini mwa jimbo hilo la California kuanzia Ijumaa, jambo ambalo limezua maandamano makubwa.
Uvamizi huo wa siku mbili umesababisha kukamatwa kwa watu zaidi ya 100, na kuchochea maandamano ya watu wenye na hasira ambao wamekuwa wakikabiliana na maofisa wa serikali kwa mabomu ya machozi, maguruneti moshi na mawe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma