

Lugha Nyingine
Shughuli za utalii za siku za lavender zahimiza maendeleo ya uchumi katika Mkoa wa Xinjiang, China (5)
Maua ya mimea ya lavender yamechanua vizuri kwenye mashamba makubwa mwezi Juni katika Wilaya ya Huocheng ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, China, ambapo mandhari ya mashamba hayo yanaonekana kama bahari kubwa ya rangi ya zambarau inayopendeza.
Shughuli za utalii za siku za lavender zinahusisha sanaa za maonesho, mashindano ya michezo, na maonyesho ya mali ya urithi huko. Shughuli hizo zimeanza rasmi jana Jumapili ili kwenda sanjari na mandhari hayo ya kuvutia sana ya mazingira ya asili, kuonesha shughuli zinazostawi za mimea ya lavender ya mkoa huo wakati huohuo, na kuhimiza maendeleo ya shughuli za utalii na uchumi za huko.
Wajenzi waendelea kujenga daraja refu zaidi duniani katika Mkoa wa Guizhou wa China
Majira ya kuvuna mazao ya mpunga yawadia katika Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China
Migodi iliyotelekezwa yageuzwa kuwa vivutio vya kitalii katika Mkoa wa Shandong, China
LEGOLAND Shanghai Resort kuanza shughuli za majaribio kabla ya kufunguliwa Julai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma